Ni mwanamziki anayekuja vizuri kwenye Tansia ya muziki
wetu wa bongo fleva ambapo mpaka sasa amechi single kadhaa ikiwa ni pamoja na
ile ya Mziki mtamu ila dada huyu ana mengi ya kusema sasa msikilize hapa..




Ninachojua penye nia pana njia na ukikazana mafanikio
yanakuja kwa wakati wake, nikiwa naendelea kuandika mashairi ya nyimbo zangu
bado napanga mbinu nyingi za kukabiliana na mziki wa bongo, mwanzo nilipo anza
rasmi kurecod haikuwa ngumu sana kwangu coz nilipokelewa vizuri kila studio
niliofika na wamekuwa wakionesha mchango mkubwa kwangu kwa vitu vingi,.Kunakitu
kina weza kukutokea katika maisha na ukakiwasilisha kwa jamii kwa njia ya
muziki, mara nyingi napenda kuimba maisha yetu ya kawaida na mambo mengine
ninayokumbana nayo nikiwa kama msichana.

Natarajia kuachia nyimbo yangu karibuni na pia ntashukuru
mungu endapo watanzania watanielewa na kunipokea kwani muziki bila mashabiki
hakuna chochote waweza fanya, Japo muonekano wangu wengi wananishauri nifanye
mitindo lakini mahisi sipo tayari kwa sasa japo napenda sana na naweza vitu
vingi vinavohusu mitindo ila daima najua kila jambo linawakati wake . kwa
mipango ya mungu nikija kufanikiwa kwenye muziki nina mpango wa kufungua
kampuni yangu ya mitindo kwani ninauwezo wa kuchora nguo na kushona pia
kudizaini vitu vingi vinavohusu urembo, Najua kwa kufanikisha hili nitaweza
kuitangaza nchi yangu vizuri sana kitaifa na kimataaifa kupitia muziki na
mitindo

Pamoja na kujua kuimba bado ninauwezo mkubwa wa kudance
aina nyingi za muziki wa mataifa mbalimbali pia nimejifunza mengi kuhusu
dancing maana nategemea itanisaidia sana katika muziki wangu.
Pia kaa tayari kwa ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la PENZI LAKE
Post a Comment