Msanii anayefanya vizuri kwenye upande wa bongo Saimon
Mwapagata almarufu kama ‘Rado’ amenusurika kifo kutoka kwa vijana waliofunga
njia maeneo ya Mwananyamala, jijini Dar Jumapili iliyopita.
Taarifa kutoka kwa rafiki wa karibu wa Rado ambaye pia naye
msanii wa filamu, Deogratius Shija, tukio hilo lilitokea usiku wakati Rado
alipokuwa akirudi nyumbani kwake
“Alikuta njia imefungwa na vijana watatu, alijaribu
kuwapigia honi lakini hawakufungua njia.
“Rado alishuka kwenye gari na kuwauliza kwa nini
wamefunga njia wakamjibu kwamba mmoja wao ameibiwa simu, hivyo wanamtafuta
mwizi wao.
Shija aliongeza kuwa
vijana hao walimvamia Rado na kuanza
kumpiga kwa mapanga na marungu na kusababisha rado
kupoteza fahamu.
Shija alizidi
kuongeza na kusema “Nilipigiwa simu na msamaria
na kuambiwa kuwa Rado hajiwezi, sababu kuna watu wanaomjua maeneo yale
alipelekwa Oysterbay Polisi kisha kukimbizwa Hospitali ya Mwananyamala ambako
alishonwa, kifuani na mguuni,”
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.