Mh.Peter Serukamba
Leo kutoka bungeni kimeibuka kioja cha mwaka baada ya
wabunge kuja na stail ya matusi bungeni
Mh.Peter Serukamba leo hii amesikika waziwazi bila ya
aibu kabisa akitoa tusi mbele ya bunge na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa
dhidi yake.
Alisikika akisema hivi "Come-on F.U.*.K Y.O.U."
KABLA YA KAULI HIYO KUTOKEA ILIANZIA HUKU
Hotuba ya kambi rasmi ya upinzani iliitaka serikali
iwachukulie hatua kali wahusika wote wanaohusika na matukio ya utekwaji na
uteswaji wa baadhi ya watu,kwa kutolea mifano ya Dr.Ulimboka na Kibanda.katika
hotuba hiyo,kambi imeonesha kutoridhika na mwendendo wa utendaji wa idara ya
usalama wa taifa.
Aidha hotuba hiyo kuna mahali imemtaja Rwakatare na
mwenendo wake kabla ya kukamatwa.
Shida imeanza pale ambapo Mh.Serukamaba aliomba mwongozo
wa spika,na kusema kuwa,kuna baadhi ya maswala yaliyomo ktk hotuba hiyo (hasa
kuanzia ukurasa wa 1-4) yanazungumzia kesi ya Rwakatare ambayo tayari ipo
mahakamani.
Na kwamba kuendelea kusomwa kwa hotuba hiyo ingekuwa ni
kuingilia mwenendo wa kesi na kwamba hapo ingekuwa ni kuingilia uhuru wa
mahakama.
Katika kutetea hoja zao,wabunge watatu wa kambi ya
upinzani(H.Mdee,J.Mnyika na T.Lisu) walisimama na kujaribu kuonesha uhalali wa
hoja zao.Wote watatu walijieleza kwa kadiri walivyoona inafaa.
Baada ya hapo ndipo aliposimama Mh.Serukamba na
kusisitiza uhalali wa hoja yake.
Sasa kile kitendo cha yeye kusimama tena,inaonekana
kulikuwa na minong'ono upande wa pili(lakini hiyo haikusikika) ndipo alipojikuta
akiropoka maneno hayo hewani tena
bungeni "Come-on F.U.C.** Y.O.U."!
Kwa jinsi alivyotukana,aliunganisha haraka na maelezo
yake kiasi kwamba Mh.J.Ndugai(aliyekuwa akiongoza) hakumkatisha, akamwacha
aendelee.
Baada ya maelezo ya Mh.Serukamba,naibu spika(mwenyekiti)
alitoa kauli yake rasmi.
Ndugai amesema kuwa mgogoro huu una mtazamo wa
kikanuni,kwa hiyo ameagiza kamati ya kanuni ya bunge ikutane mara moja kujadili
swala hilo kisha itoe ushauri kwa kiti cha spika jinsi gani ya kshughulikia
mambo hayo yanayoonekana yana utata.
Aidha amesema hotuba hiyo ya kambi rasmi ya upinzani
itaendelea kusomwa kipindi cha jioni.
Post a Comment