Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu Mkuuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.Rwekaza Sympho Mukandala amesema hayuko tayari kubadili matokeo ya Kidato cha Nne.

Chanzo cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya kutolewa taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa. 'Sisi tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao.

Iweje leo Baraza libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na kwa ustawi wa elimu ya wapi?' alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala.

Habari za kuaminka zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi wake huo.

Post a Comment

  1. huo ndo uzalendo, serikali ilikurupuka

    ReplyDelete
  2. waachie ngazi tu waondoke kwani hao wanafunzi waliofanyiwa mabadiliko bila taarifa unadhan wanajiskiaje?. Inauma sana kitendo cha wadogo ze2 kufanyiwa hvy lakn kwaasie husika atanyanyua mdomo tu. kama wamegundua wanaangamiza kizazi kwanini wasifanye marekebisho, nyie kama hamtaki kwendeni uko watoto wenu ni vile wanasoma nje ndomaana haiwaumi.

    ReplyDelete
  3. Dawa ya moto ni moto. Nadhani ukweli haujajulikana kwa nini Waziri mkuu kupitia tume yake waagize matokeo yafutwe. Kama ni suala la ubabaishaji katika utendaji hawa wangefunguka wazi waseme kama ni kuburuzwa waaachie ngazi na waeleze kusudi watanzania ambao wanadukuduku waelewe. Hatutaki kuingizwa kwenye utata.

    ReplyDelete

 
Top