MKONGWE kwenye sanaa Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa
endapo ikitokea mkurugenzi mwenzake, Vincent Kigos akaoa, yeye
atajitolea kuwa mwandaaji wa chakula.
Akizungumza na mwanahabari wetu mwishoni mwa wiki iliyopita, Johari
alisema yeye na Ray ni watu wa karibu kwa kuwa wameiongoza kampuni yao
kwa muda mrefu hivyo katika jambo muhimu kama la ndoa, lazima ajitoe
kinaga ubaga kufanikisha.“Yani hata kama ikitokea kesho mkasikia Ray anaoa ujue kabisa nitakuwa muandazi kuhakikisha madikodiko yanawafikia waalikwa kwa wakati muafaka,” alisema Johari ambaye mara zote amekuwa akikanusha kuwa uhusiano wa
Post a Comment