Mfanyabiashara
mwanamke wa Kighana (pichani) amekamatwa na kilo 10 za Heroin wakati
akitokea Tanzania. Mercy Agyeman Prempeh (36) amekamatwa katika Uwanja
wa Kimataifa wa Ndege wa Kotoka wakati akitokea Tanzania. Polisi
walimtaka mwanamke huyo kutambua mizigo yake uwanjani kutokana na sehemu
aliyokuwa anatokea yaani Tanzania.
Baada
ya kuhojiwa na polisi alidai kuwa rafiki yake wa Kitanzania ndiye
aliyempa mzigo huo ampelekee mtu asiyejulikana anayeishi katika jiji la
Accra kwa ada ya Dola za Kighana 2,500. Amedai mwenye mzigo alitakiwa
akutane nae hapo airpot na kumpatia kiasi hicho cha fedha lakini
anaamini amengia mitini baada ya yeye kukamatwa.
Post a Comment