Kufuatia ombi la mheshimiwa Mnyika kwa Spika Ana Makinda leo asubuhi bungeni, Ana Makinda amejibu kuwa mpaka sasa hakuna kesi yoyote iliyofunguliwa inayohusu kusimamisha ripoti ya CAG na TAKUKURU isisomwe bungeni, akishangiliwa kwa kelele na vifijo Makinda amesema kuwa hata zile kesi 10 zilizokuwazinasemwa kuhusu IPTL hazipo hivyo ripoti itasomwa kama ilivyopangwa kesho Jumatano.

Itakumbukwa kuwa wiki iliyopita Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliropoka bungeni kuwa yeye amesoma sheria hivyo anashauri busara itumike ili suala hili lisijadiliwe kwa kuwa kuna kesi mahakamani.

Post a Comment

 
Top