Staa wa filamu za kibongo anayejulikama Aunty Lulu ambaye amecheza kwenye filamu kama Lost Soul amefunguka makubwa likiwemo tukio la yeye kubakwa na rafiki wa shemeji yake (rafiki wa mume wa dada yake) nakupoteza ndoto zake za kuolewa

Msanii huyo ambaye wakati anasoma Kisuti Girls Secondary alikwa akiishi kwa dada ambapo rafiki wa mume wa dada yake huyo alikuwa na mazoea ya kufika nyumbani kila wakati alipokuwa akifanya kazi maeneo ya Posta jijini Dar,ambapo mwanaume huyo alikuwa na mazoea ya kujakumpa lifti msanii huyo mpaka nyumbani kwa dada yake alipo kuwa akiishi msanii huyo ndipo siku moja jamaa huyo alijaribu kumrubuni ili wafanye mapenzi lakin msanii huyo alikatakata kwa madai ya kwamba alikuwa bikra hivyo hataka kuhfanya dhambi
nakuu alicho kisema hizi ni sentesi zake nne akielezea machungua nayosikia 


“Kwa kawaida yule jamaa alikuwa akinifikisha nyumbani kwa dada yangu pale Makumbusho (Dar), ananisubiri, nabadilisha nguo, naenda naye kwake maeneo ya Block 41 (Kinondoni) ambako alikuwa akinifundisha. So alinibakia nyumbani kwake,”

“Huwa najisikia kulia kwa sababu huyo rafiki wa shemeji yangu alinipotezea ndoto nilizokuwa nazo kwamba nitafanya juu chini niolewe nikiwa ‘mbichi’ hivyo mapenzi ningefanya nikiwa ndani ya ndoa.

“Sikufurahia kabisa kitendo hicho maana naona pia kiliniathiri kisaikolojia,” alisema Aunty Lulu.

“Baada ya tukio lile aliomba anioe ili nimsamehe lakini nilikataa. Baadaye alikwenda kusoma nje ndipo tukapotezana na sijawahi kumuona tena, nasimulia ili liwe fundisho kwa wanawake wanaopenda kuwa na ukaribu kupitiliza na wanaume wasiowajua kiundani,” 


Post a Comment

 
Top