Nyota wa Barcelona, Lionel Messi Jumatano usiku aliendelea kuvunja rekodi baada ya kupachika bao lake la 76 kwenye dimba la UEFA na kufikia rekodi ya mfungaji bora iliyokuwa ikishikiliwa na mkongwe wa Real Madrid, Raul Gonzalez.Messi aliisaidia Barcelona kumaliza ya kwanza kwenye kundi F, kwa kuilaza PSG 3-1 ambapo alichangia bao moja hukue mengine yakitingwa na Neymar pamoja na Luis Suarez.Rekodi hiyo ya Messi inajiri wiki chache tu baada ya fowadi huyo kufuta nyingine ya Raul na kuwa mfungaji bora wa nyakati zote katika ligi kuu ya Uhispania La Liga.
Huku Raul akiwa kastaafu, Messi sasa atapambana na hasimu wake Cristiano Ronaldo katika kuboresha zaidi rekodi hiyo, ambaye kafunga magoli 75 kwenye UEFA.Filippo Inzaghi ambaye kwa sasa ni kocha wa AC Milan, ndiye wa tatu kwenye orodha ya rekodi hiyo akiwa na jumla ya mabao 70 mbele ya Mjerumani Gerd Muller 69, ambaye pia ni mstaafu.Kwenye mechi hiyo, straika wa Sweden Zlatan Ibrahimovic aliiweka mbele PSG lakini dakika nne baadaye Messi akasawazisha na bao lake la 76 kabla ya kuwapisha Neymar na Suarez kumalizia.
Post a Comment