Sidhani kama ulikuwa unajua kama Ghana mtu akifa ni huzuni lakin kwao pia ni kusherekea kwa kuwa wanaamini kwamba mtu akifa huwa anaenda kwenye maisha mengine kabisa, Hivyo ndivyo ilivyo kule nchini Ghana ukifa lazima uzikwe kwa aina kipekee ikiwa ni pamoja na jeneza ambalo litahusika kupumzisha mwili wa marehemu.
Kwa hapa kibongobongo tumezoea tu kwamba mtu ukifariki tunazika kwenye jeneza la mbao na lenye style moja lakin ghana wao wameendelea wafikia mpaka hatua ya kutengeneza majeneza ambayo yana umbo la gari kama benz,chupa ya coca cola na mengine mengi tu
Picha hizi hapa chini ni baadhi ya majeneza ambayo yanatengenezwa Ghana ambayo yanauzwa kati ya dola za kimarekani 500-600
Post a Comment