breaking news


Mnamo Tarehe 22 Januray mwaka huu majira ya saa tanio usiku huko kijiji cha Songambele wilaya ya Mlele,mkazi mmoja ambaye jina lake ni  Richard Madirisha kabila lake msukuma, 31 aliyekuwa akijulisha na shughuli za kilimo, akiwa amelala na mke wake ghafla alivamiwa na watu wasiojulikana karibia watano ambapo walivunja mlango na kuingia ndani na kuanza kumkatakata mapanga, kutenganisha kichwa, sehemu za siri kisha kuchemsha viungo hivyo nje ambapo moto ulikuwa unawaka.

Sufuria za kuchemshia viungo hivyo walivichukua ndani ambapo walimtishia mke wa marehemu aitwaye Mekrina Moses, msukuma, 25yrs asipige kelele.

Baada ya kukamilisha zoezi walinawa mikono kwa kutumia sabuni iliyokuwa nyumbani kwa marehemu na kuondoka na simu ya marehemu

Taarifa za awali inaonyesha chanzo kulipiza kisasi kwani marehemu alikuwa akiishi Kaliua mkoani Tabora na huyo mwanamke alikuwa ni mke halali wa Shija Manyama wa kaliua hivyo marehem alipora.

Kitendo hicho kilimuudhi Shija na kuamua kukata mapanga ng'ombe 7 wa marehemu na ugomvi ukawa unaendelea hadi July 2014 ambapo marehemu alihamia kijiji cha Songambele wilaya Mlele, na hata hivyo inasemekana vitisho viliendelea kutolewa na Shija dhidi ya marehemu kwa njia ya simu.

Jitihada za kuwatafuta watuhumiwa zinaendelea.

Credit Jamii Forums

Post a Comment

 
Top