Movie bado inaendela huku Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akiwa tayari mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa mahojiano na tarifa zingine zinakuja na kudaku kuwa Askou huyo kupoteza fahamu kutokana na mshutuko, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amemtaka Askofu huyo aripoti ofisini kwake keshokutwa kutoa maelezo kuhusiana na tuhuma za kumkashifu kiongozi mwenzake wa dini.



Makonda, ambaye kwa nafasi yake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, amemwandikia barua Askofu Gwajima akimtaka kufikia ofisini kwake kutoa ufafanuzi juu ya maneno makali dhidi ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki.

Katika barua yake, Makonda alisema ofisi yake inataka kufahamu kama uhuru wa kuabudu kikatiba ni kutokuheshimu watu wengine. “Hatuamini kama imefika wakati kwenye nyumba za ibada kumegeuka sehemu ya kutukana na kuwasema watu badala ya kuhubiri habari njema. Tunataka kujidhihirisha malengo hasa ya kutumia maneno hayo ni nini.”Anadaiwa kuzimia jana alipokuwa akihojiwa na Polisi kwa tuhuma za kumkashfu Kardinali Pengo.


Credit Dar24

Post a Comment

 
Top