Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza kuendelea kushuka kwa bei ya mafuta bei ambazo zinaanza kutumika Jumatano hii.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo, Ewura imesema katika bei hizo mpya, sasa mafuta ya petroli imeshuka kwa Sh 116 kwa lita moja, dizeli Sh 145 na mafuta ya taa Sh 134 kwa lita moja.
Katika taarifa hiyo imesema kwamba bei za sasa ni Sh 1,652 kwa lita moja ya petroli, Sh 1,563 kwa lita moja ya dizeli na Sh 1,523 kwa lita moja ya mafuta ya taa bei ambazo zinaanza rasmi leo.
Kwa mujibu wa EWURA, punguzo hilo la bei linaonesha kwamba hakuna mkoa ambao utauza nishati hiyo kwa Sh 2,000 na hivyo kutoa unafuu mkubwa katika mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na unafuu wa usafirishaji wa bidhaa.
Wananchi watakaonunua kwa bei ya juu nishati hiyo ni wa Uvinza mkoani Kigoma ambao watanunua kwa Sh 1,895 kwa lita moja ya petroli, Sh 1,806 kwa dizeli na Sh 1,766 kwa mafuta ya taa.
Ewura imesema hata hivyo bei hizo hazijashuka sana kutokana na kuendelea kushuka thamani ya shilingi ambayo kuanzia Desemba mwaka jana imeshuka kwa asilimia 8
Post a Comment