Mmiliki wa kampuni ya kutengeneza kompyuta ya Microsoft, Bill Gates.

Bwanyenye mmiliki wa kampuni ya kutengeneza kompyuta ya Microsoft , Bill Gates, ndiye tajiri nambamoja duniani kwa mwaka wa pili mfululizo.
Kwa mujibu wa takwimu za jarida la Forbes ambalo huchapiShwa mara moja kila mwaka, Bill Gates ameorodheshwa kumiliki zaidi ya dola bilioni 79.2.

Mfanyibiashara kutoka Mexico, Carlos Slim Helu.

Mfanyibiashara kutoka Mexico Carlos Slim Helu ameorodheshwa tajiri nambari mbili duniani akiwa na zaidi ya dola bilioni 77.1. Kulingana na jarida hilo, Gates alipata faida kubwa ya dola bilioni $3bn mwaka uliopita.

Warren Buffett.

Hadi kufikia sasa kuna matajiri 1,826 wenye utajiri unaozidi dola bilioni moja kote duniani hii ikiwa ni ongezeko la mabilionea 181 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Gates ameorodheshwa nambari moja duniani katika miaka 16 kati ya 21 zilizopita.
Bwanyenye mwingine kutoka Marekani, Warren Buffet, anaorodheshwa katika nafasi ya tatu akiwa na dola bilioni $72.7

Amancio Ortega.

Mwanzilishi wa mitindo ya nguo ya Zara, Amancio Ortega, kutoka Uhispania anashika nafasi ya nne duniani.

Larry Ellison.


Mfanya biashara namba 1 Afrika, Aliko Dangote.

Orodha ya Forbes ya 2015 ya matajiri zaidi duniani.
1. Bill Gates $79.2bn (Microsoft)
2. Carlos Slim Helu $77.1bn (Mfanyabiashara Mexico)
3. Warren Buffett $72.7bn (Mfanyabiashara)
4. Amancio Ortega $64.5bn (Mwanzilishi wa maduka ya nguo ya Zara )
5. Larry Ellison $54.3bn (Kampuni ya teknolojia ya Oracle)
6. Charles Koch $42.9bn (Mfanyabiashara)
7. David Koch $42.9bn (Mfanyabiashara)
8. Christy Walton $41.7bn (Mmiliki wa maduka ya Walmart)
9. Jim Walton $40.6bn (Mmiliki wa maduka ya Walmart)
10. Liliane Bettencourt $40.1bn (Muuzaji wa vipodozi L'Oreal )

Hii ni orodha ya matajiri wanaoongoza Afrika na thamani ya mali walizonazo:
1. Aliko Dangote (Nigeria) $14,700,000,000
2. Johann Rupert (Afrika Kusini) $7,400,000,000
3. Nicky Oppenheimer (Afrika Kusini) $6,700,000,000
4. Nassef Sawiris (Misri) $6,300,000,000
5. Christoffel Wiese (Afrika Kusini) $6,300,000,000
6. Mike Adenuga (Nigeria) $4,000,000,000
7. Mohammed Mansour (Misri) $4,000,000,000
8. Nathan Kirsch (Swaziland) $3,800,000,000
9. Issad Rebrab (Algeria) $3,400,000,000
10. Isabel dos Santos (Angola) $3,300,000,000


Watanzania walioingia kwenye orodha ya mabilionea ni Mohammed Dewji na Rostam Aziz.

Post a Comment

 
Top