Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo la jijini Dar, Josephat Gwajima ambapo siku chache zilizopita alirekodiwa huku akimtusi Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini, Polycarp Kardinali Pengo, sasa taarifa mpya ni kuwa mchungaji huyu ametumwa kuchafua kwa matusi jina la Kadinali Pengo.


mchungaji gwajima



Taarifa kutoka Global Publishers zinasema

Gwajima alirekodiwa kwenye ibada ya kanisa lake Jumapili iliyopita ambapo ‘alimtusi’ Pengo akituhumu kuwa ni msaliti kwani amekwenda kinyume na Taasisi ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza la Makanisa ya Kipentekoste (CPCT) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa kuwataka waumini waisome Katiba Inayopendekezwa kisha wapewe uhuru wa kupiga kura ya “ndiyo” au “hapana” tofauti na vyombo hivyo vyenye dhamana ya kuongoza dini ya Kikristo vilivyotaka waumini waipigie kura ya “hapana” Katiba Inayopendekezwa.

Chanzo cha Habari kilichoipa taarifa hii Global kinasema kuwa

“Gwajima anatumika tu anamkashifu Pengo ili kumchafua na asiweze kusimamia hoja yake ya kuwaacha wapigakura waamue wenyewe kuikubali au kuikataa Katiba Inayopendekezwa wakiamini watu wanaweza kuipigia kura ya “ndiyo” na suala hilo likajadiliwa wakati wenzake wamelipinga,” 

“Siyo tu kuhofia Mahakama ya Kadhi, Gwajima ametumika kumchafua Pengo kwa hofu kuwa huwenda akawa ana mgombea wake anayemtaka awe rais,” 

Baada ya Hapa Global walifanya Jitihada za kumsaka Mchungaji huyo lakini hazikuzaa matunda na simu yake ilipokelewa ilijibu kama ifuatavyo

“Mchungaji (Gwajima) ametumwa na Roho Mtakatifu kusema yale aliyoyasema hakutumwa na mtu wala kikundi chochote cha wanasiasa,” 


Hii Vita ya kidini imetoka wap tena

Post a Comment

 
Top