Baada ya Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kukataa tuhuma za kuwa alihusika katika kusambatisha ndoa ya Muimbaji wa Injili Flora Mbasha na mumewe, Emmanuel Mbasha sasa baada ya Gwajima kukamatwa na polisi akishutumiwa kumtusi Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycap Kadinali Pendo, Emanuel Mbasha naye aja juu na kudai kuwa malipo ya dhambi alizofanya na kuwa itaendelea hivyo mpaka atakapoacha dhambi zake.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka mtandao wa Global Pulisher walimpigia simu Emanuel Mbasha na alikuwa na haya kusema
“Ile hali (kupoteza fahamu) ya Gwajima ni malipo. Mimi nilishasema jamani, mtu akikutendea ubaya malipo ni hapahapa duniani, hakuna kwingine,Mimi ndoa yangu haipo, mke wangu anajua yeye anavyoishi. Kwa hivyo mimi nimekuwa nikiishi kwa manung’uniko kila siku, unadhani nini kitatokea kwake?”Tena namwomba Mungu ampe afya Gwajima, akitoka hospitali alikolazwa (TMJ, Dar) anitafute kuniomba msamaha,Ni vyema na itakuwa vyema zaidi akinitafuta na kuniomba msamaha ili kila mmoja aishi kwa amani. Mimi nisiwe na kinyongo na yeye na wala yeye asiwe na kinyongo na mimi.Hilo atajua yeye mwenyewe na Mungu wake, mimi sijui. Ila ninachojua mimi ni kitu kimoja tu, kwamba Mungu amenilipia basi, sasa aniombe msamaha.”
Baada ya taarifa hizi kusambaa sana sasa habari mpya ni kwamba kuna uwezekano kuwa, huenda serikali ikalifungia kanisa lake lililopo Kawe jijini Dar,
Unafikiri waumini wa kanisa hilo watakubali kufungwa kwa kanisa lao au ni Story tu?
Post a Comment