Baada ya uhusiano wake kuvunjika na msanii wa Bongo Fleva, Malick Bandawe Msanii wa Filamu kutoka Industry ya Bongo Movie, Rose Ndauka ambaye kwa sasa amekuwa akivicha sana story za yeye anatoka na nani lakini kwa taarifa zilizopo ni kwamba yupo kwenye Penzi zito na mtayarishaji wa Muziki Producer Emmanuel Saimon Sewando maarufu kama Manecky.
Wawili siku za karibuni wamekuwa wakiwa pamoja muda mwingi kwenye kumbi mbalimbali za starehe nyakati za usiku pamoja na studio ambayo Manecky anafanya shughuli zake za kutayarisha mziki shuhuda mmoja aliuambia mtandao wa Global kuwa
"Rose na Manecky ni wapenzi kwani muda mwingi wako pamoja, wanaongozana kama kumbikumbi hasa usiku. Huwa tunawaona wanakuja maeneo ya hapa Afrika Sana wanakwenda kununua chakula cha jioni huku Manecky akijinadi kuwa ameamua kuwa na Rose kwa kuwa mke wake halali hivi sasa ni mjamzito,”
Lakini cha Ajabu baada ya wawili hao kuulizwa kuwa kama wanadate walikanusha na hii ni kauli ya Manecky
“Ukaribu wangu mimi na Rose ni kazi tu kwani kuna ‘project’ tunaifanya nadhani mwenyewe Rose ndiyo anaweza kuweka wazi hilo, kingine Rose anafanya kazi na mdogo wangu kwenye gazeti la Rozzie la mtandaoni,”
Licha ya mke wa Manecky kuwa mjamzito watu wanadai kuwa Manecky ameamua kutembea na Rose kwa kuwa mkewe hampi chakula cha ndoa
“Hamna kitu kama hicho jamani.”
Rose Ndauka naye akaruka futi mia mbili kwenda juu kuwa hatembei na Manecky?
“Hakuna kitu kama hicho jamani, kwani mimi nachaguliwa mtu wa kukaa naye? Acheni kusikiliza maneneo ya watu halafu Manecky ana mke ambaye ni mjamzito na anatarajia kujifungua muda wowote,”
Ukaribu wa Rose na Manecky kweli unaletwa na kazi?kama ni kazi ipi Muziki au Filamu, au Rose naye kaingia kwenye Bongo Fleva?
Related Posts
- Alikiba Apost Picha Kuonyesha Ukubwa wa Mimba ya Wema Sepetu.27 Jan 20160
Wema Sepetu Week Mbili Hizi Amekuwa kwenye Headlines sana ikisemakana kuwa Anaujauzito wa Msh...Read more »
- Baada ya Shamsa Ford Kuachana na Nay Huyu Ndie Aliyeziba Pengo.21 Nov 20150
Staa Nay Wa Mitego Baada ya Kuacha na aliyekuwa Mpenzi wake Shamsa Ford najua utakuwa mfuatilia...Read more »
- Uhusiano wa Kimapenzi Kati ya Idris Sultan na Samanthan Umevunjika.21 Nov 20150
Big Brother Africa Hotshots winner Idris Sultan ambaye kwa sasa yuko Mbioni kuanza Show yake mp...Read more »
- Jokate Anasa Ujazito wa Alikiba.07 Nov 20150
Staa Jokate Mwagelo ambaye kwa sasa yuko Mapenzini na Staa wa Muziki wa Kizazi Kipya Ali Kiba...Read more »
- Picha za Wema Sepetu Afunga Ndoa na Luis Munana wa Namibia.29 Oct 20150
Wema Sepetu amefunga ndoa kwa mara ya pili mwaka huu – kwenye movie bila shaka! Baada ya miezi ...Read more »
- Video ya Shilole Ana Mimba ya Nuh Mziwanda.26 Oct 20150
Tetesi za Hapa na pale ni baada ya kusika kuwa Msanii Shilole ana Ujazito wa Mpenzi wake Nuh Mz...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.