Chagga Barbie demu wa nay wa mitego sasa hivi

Staa Nay Wa Mitego Baada ya Kuacha na aliyekuwa Mpenzi wake Shamsa Ford najua utakuwa mfuatiliaji Mzuri kwenye akaunti yake ya Insta lakin nina hakika utakuwa hujaona viashiria vyoyote kuwa na Mpenzi mpya.

Chagga Barbie sio jina geni, ndio yule aliyezitawala headlines nyingi alipokuwa mpenzi wa Prezzo, jina lake halisi ni Starlisha Tillya lakini sasa anatumia jina la Chagga Empress Instagram.

Chagga Barbie Starlisha Tillya


Nay na Chagga ambaye ni Mtanzania aishiye Marekani wamekuwa wakiweka post zinazoashiria kuwa kuna kitu kinaendelea kati yao zaidi ya urafiki wa kawaida, lakini Nay amesisitiza kuwa hawajaingia kwenye ukurasa wa mahaba japo Nay amekiri kuwa anampenda sana Chagga Barbie.

Novemba 11, Chagga alipost video akisema anampenda Nay, na Nay aliirepost na kuandika “Love you too bby Mtag umpendae @chaggaempress @chaggaempress”.



“Naomba tu watu wajue ni mwanamke ambaye ninampenda, nampenda the way alivyo ni mwanamke mzuri anavutia sio vinginevyo, labda ikija ikatokea akiwa mwanamke wangu itakuwa ni poa zaidi lakini for this time nampenda the way alivyo” Nay ameiambia Bongo5.

“Mimi na Shamsa tulishaachana muda mrefu tumebaki washkaji ana bwana yake nafikiri watu wanaona kwenye page yake anampost, lakini mwisho wa siku nafasi ikishaachwa na mtu watu watajua wataona tu dalili, for this time sidhani kama natakiwa kuongea mengi sana nafikiri watu wataona, lakini watu wajue kwamba Chagga ni mwakamke ambaye nampenda namkubali amekuwa ni rafiki yangu wa karibu sana, ni mwanamke mzuri so haijafikia hatua ya kuwa na mahusiano ya kihivyo ila ikifikia watu wataona coz tuko karibu.” Alisema Nay.

“Nafikiri tutakutana hivi karibuni, hivi karibuni tutakuwa pamoja bado hatujaonana”.- Nay


Post a Comment

 
Top