Siku chache baada ya msanii
na prodyuza wa muziki wa
kizazi kipya, Raheem Rummy
Nanji ‘Bob Junior’ kupokea tuzo kutoka
kwa aliyekuwa hasimu wake Naseeb Abdul
‘Diamond’
imebainika kuwa
walishamaliza bifu lao
lililodumu kwa muda mrefu,
Fleva kishyma_blogspot inakuhabarisha.
Akifichua kilichokuwa
nyuma ya pazia, Bob Junior
alisema kwamba, Diamond
alimpigia simu na kumuomba
radhi kabla ya kumwalika kwenye ‘bethidei’ yake
iliyofanyika Oktoba 2,
mwaka huu katika Klabu
Maisha jijini Dar. “Diamond alinipigia simu na
kutaka tuyamalize na nishiriki
katika sherehe yake ya
kuzaliwa, nikatafuta ushauri
kwa vijana wakanitaka
nimpotezee lakini wazee pamoja na mama yangu mzazi
wakaniambia nimsikilize na
kushirikiana naye, nami
nikaukubali ushauri huo wa
wazee,” alisema Bob Junior.
Prodyuza huyo ambaye alidaiwa kugombana na
Diamond kwa kudaiwa
kumkatalia kumfanyia kazi
yake, alisema kuwa sasa
tofauti zao zimekwisha na
wanajiandaa kufanya kazi pamoja.
Diamond alisherehekea siku
yake ya kuzaliwa kwa
kuwazawadia tuzo watu
mbalimbali waliofanikisha
uwepo wake katika muziki na kumvisha pete ya
uchumba mpenzi wake
anayetamba katika filamu,
Wema Sepetu.

Post a Comment

 
Top