![]() |
MSANII OMMY DIMPOZI KUTUA MISS REDDS TABORA 2013/14 |
![]() |
Sarahy Paul mshindi wa mwaka jana 2012
Mashindano ya Miss Redds Tabora kukujia tena kwa sura pevu
zaidi, hii ni baada ya kufanyika mashindano kama haya mwaka jana na kufanikiwa
kwa kiasi kikubwa, sasa ni zamu nyingine yaliyonuwiwa kuwa na ubunifu wa
kutosha kwa maandalizi kabambe yaliyofanywa tayari kuanzia sasa.
Nikiwasiliana kutoka SPAIN BARCELONA na muandaaji wa
mashindano haya kwa miaka minne (4) sasa mfululizo toka akabidhiwe kutoka kwa
muandaaji wa zamani Mbunge wa sasa mjini Tabora Mh. Rage chini ya V.O.T FM
Mgalula Fundikira ambaye kwasasa ni wakala aliyepewa tena idhini ya kuyaandaa
shindano hili kutoka kwa LINO INTERNATIONAL wenye hati na idhini ya kuandaa
mashindano haya toka ngazi za vitongoji hadi mashindano makubwa ya MISS
TANZANIA.
"....uwakala wangu unaendelea baada ya kuombwa na
LINO INTERNATIONAL kuandaa tena mwaka
huu na sasa hivi na msanii Ommy Dimpoz na msanii
atakaye mchagua yeye Dimpoz watakuwepo kutoa burudani ya kutosha..."
Alisema Mgalula akiwa Spain Barcelona.
*************
Kuhusu form za ushiriki zitatangazwa mapema wiki ijayo wapi
zitapatikana na taratibu zote za mashindano utapata kuzifahamu vizuri.
TIMIZA NDOTO ZAKO ZA KUIBUKA MREMBO WA MISS REDDS TABORA.
Nani ungependa awe msanii atakaye chaguliwa na Ommy D?
Post a Comment