Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ameachiwa kwa
dhamana hivi punde baada ya kushtakiwa kwa makosa ya uchochezi katika mahakama
ya Mkoa wa Arusha huku maandamano yakifanyika hivi sasa katika mitaa ya Jiji la
Arusha, Tanzania.
Katika Mahakama hiyo kulikuwa na umati mkubwa wa wafuasi
na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Mashabiki, wafuasi na wanachama wa chama hicho walifurika
katika mahakama hiyo kwa ajili ya kumuunga mkono mbunge huo.habarimasai.com
itaendelea kukuletea Taarifa zaidi baadaye.
Hivi sasa mashabiki, wafurukutwa na wanachama wa Chadema
wanafanya maandamano makubwa kuelekea katika ofisi za chama hicho ambazo zipo
katika eneo la Ngarenaro.
Hivi sasa wanapita katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mulongo kwa maandamano huku wakipiga kelele za kuzomea.
Kesi ya uchochezi dhidi ya Lema imefunguliwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mkoa wa Arusha na endeshwa na Hakimu Devota Msoffe.
Mwandishi wetu anasema kwamba kesi hiyo imeahirishwa
mpaka Mei 29 mwaka huu.
Katika hati ya mashtaka ambayo ipo katika mahakama hiyo
inasema kwamba kosa la Lema ni ' kutoa maneno yanayodaiwa kuwa ni uchochezi.
Endelea kusoma kihymba.com kwa taarifa mbalimbali
moto moto.
Post a Comment