Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kisheria
mtu anayetumia simu isiyosajiliwa akikamatwa anaweza kutozwa faini ya Sh500,000
au kwenda jela miezi sita.
‘‘Kwa mujibu wa kifungu cha 131 cha sheria ya
mawasiliano mteja au muuzaji wa namba
ya simu ambayo haijasajiliwa atatozwa faini ya Sh500,000 au kifungo cha miezi
mitatui’’ ilielezwa jana.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma alisema hayo
alipokutana na wadau wa mawasiliano jijini hapa jana. Profesa Nkoma alisema
namba za simu ni lazima zisajiliwe kwa mujibu wa sheria ya mawasiliano ya
elekroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010.
Ufafanuzi wa TCRA umekuja baada ya kuwapo malalamiko ya
watu wa kada mbalimbali kwamba mawasiliano yao ya simu yanaingiliwa na
kuchapishwa katika vyombo vya habari.
Katika maelezo yake ya jana, Pofesa Nkoma alisema kwa
mujibu wa kifungu cha 130 cha sheria ya EPOCA ya mwaka 2010, mtu ambaye atauza
au kutoa namba za simu bila ya kusajiliwa atachukuliwa hatua za kisheria na
adhabu yake ni faini ya Sh3 milioni na kifungo cha miezi 12.
“Katika vikao vya pamoja vilivyofanyika Aprili 4 na
Aprili 11 mwaka huu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na kampuni zinazotoa huduma
za simu za mkononi, zimekubaliana juu ya hatua za kumaliza tatizo la usajili wa
namba za simu na utaratibu wa kufungia namba zote ambazo
hazikusajiliwa,”alisema Profesa Mkoma.
Profesa Nkoma alisema kwa kushirikiana na kampuni za simu
na vyombo vya usalama imeanza kampeni endelevu ili kuwabaini wanaohusika na
uvunjifu wa sheria kwa lengo kuwalinda watumiaji wema, jamii kwa ujumla kwa
ajili ya kuimarisha usalama na kuleta maendeleo na usawa katika jamii.
Pia alisema mikakati iliyopo ya TCRA simu ambazo
hazijasajiliwa hazitafanya kazi, hivyo watu
ambao hawajajisajili waanze mchakato huo.
Alisema namba za simu zilizosajiliwa ni asilimia 93 na
asilimia 7 hazijasajiliwana kwamba asilimia iliyobaki inatakiwa kuondoka
haraka..
Post a Comment