Mwanamziki anayefanya vizuri kwenye gemu ya Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ siku za
nyuma alitoa kauli ya kuwa mchumba wake ambaye ni mtangazaji wa Runinga ya DTV, Peniel Mungilwa ‘Penny’ ana
ujauzito wake na kwamba amemnunulia ‘mkoko’ (gari) la mamilioni ya shilingi kwa
ajili ya kwenda nalo kliniki kama utakuwa mfutaliaji mzuri wa story zetu basi
utakuwa umeshaisoma hii sasa Penny ameifungukia kauli hiy
Baada ya penny kulizwa juu ya ujazito wa Mwanamziki
Diamond alioneka kushangzwa sana na kauli hiyo na kupaniki ghafla
Alisema amekuwa akisoma habari za ‘mimba’ yake kupitia
magazeti lakini hajawah kuulizwa na mwandishi yeyote, jambo linalomshangaza
sana.
Na hivi ndivyo ilivyo kuwa katika maongezi na mwandish
kutoka GPL
Penny alisema: Namshangaa! Ni mimba ipi kwanza?uhusiano
wangu na Diamond unaninyima raha kutokana
na maneno ya watu.
Penny: Mh! Yaani sijui hata niseme nini, nashangazwa sana
na hizi habari, nazisikia tu halafu mimi mwenyewe mhusika sijapewa nafasi ya
kuzungumza.
Unajua sijazoea maisha haya ya kila wakati kuzungumza na
waandishi. Naomba mniache, nani aliwaambia kuwa mimi nina mimba?
Funguka: Diamond.
Penny: Kama ni Diamond muulizeni yeye mwenyewe! Mbona
nakosa raha jamani?
Funguka: Vipi mna mpango wa kuoana na Diamond?
Penny: (kwa hasira) Hizo ni ishu zangu binafsi, kama
tutaoana au hatuoani ni mipango yetu, sioni sababu ya kutangaza kwenye media.
Funguka: Unaichukuliaje kauli ya mama mkwe wako, yaani
mama Diamond? Inadaiwa alisema hatambui uhusiano wowote wa mtoto wake na
mwanamke mwingine hadi atakapofunga ndoa.
Penny: Tafadhali sana, sitaki kuzungumzia habari kuhusu
mama Diamond. Kwa hilo ‘no comment.’
Funguka: Vipi lakini, unainjoi kuwa na uhusiano na
Diamond?
Penny: (Akakata simu).
Funguka: Haloo… haloo!
Hata hivyo mapaparazi wetu walipojaribu kumpigia simu
tena hakupokea licha ya kuita kwa muda mrefu mpaka kukatika yenyewe.
Post a Comment