Habari
zilizotufikia toka IFM- Dar es salaam ni
kwamba mwanafunzi mmoja ambaye
bado hatujafanikiwa kulipata
jina lake amefariki
dunia kwa kulishwa
sumu katika chakula
alicholetewa na mpenzi
wake ambaye ni
mke wa mtu......
Taarifa zaidi zinadai
kwamba Mwanafunzi huyo alikuwa na uhusiano wa karibu sana na mke wa mtu
ambaye mbali na
starehe za kimapenzi
alikuwa pia anampekea
chakula cha jioni
Baada ya
mchezo huo kudumu
kwa muda, mume wa mwanamke
aliusoma mchezo mzima
na kuandaa tego
la kuwaangamiza wote....
Habari
zinadai kwamba Siku ya jumatano jioni mwanaume huyo aliwahi
kurudi nyumbani na
kufanikiwa kukinasa chakula
kilichokuwa kimeandaliwa tayari
kwa kupelekwa kwa
huyo mwanafunzi ambaye
alikuwa anatembea na mke
wake.....
Baada ya kukinasa, alijifanya kuzuga
na kupotezea...Mkewe alipotoka
alikichukua na kukitia
sumu chakula hicho
na kisha kukiweka
kama kilivyokuwa kimeandaliwa....
Lengo lake lilikuwa
ni kuwamaliza wote
maana alijua ni
lazima akifika watakaa na kula pamoja.....
Mwanamke alipopeleka chakula hakukaa
kula na badala
yake alimwambia yule
mwanafunzi kuwa mume wake amewahi kurudi siku hiyo
hivyo hatoweza kukaa
wale pamoja....Mwanafunzi huyo
akakipokea na kukila
na ndipo mauti
yakamkuta
Habari toka chuoni
hapo zinadai kwamba
mwanafunzi huyo alikuwa
ameshadisco lakini alikuwa
amepewa nafasi nyingine
ya kurudia mwaka
wa pili , hivyo aliendelea kukaa
mtaani kama mwanafunzi....
Mwili wa marehemu bado uko Muhimbili kwa uchunguzi zaidi
baada ya polisi kuuzuia kuzikwa....
Hizi ni habari
mbaya sana kwa
wanafunzi wa chuo
hicho maana ni jumatatu tu mwanafunzi mwingine alifariki
katika hali ya
kutatanisha baada ya kifo cha
mpenzi wake miezi
michache iliyopita....
Habari za ndani zaidi zinadai kuwa toka
mwaka huu uanze
mpaka sasa chuo cha IFM kimepoteza wanafunzi 12 huku wawili
wakiripotiwa kuwa na
hali mbaya zaidi
katika hospitali ya Muhimbili....
Soure Mpekuzi
Post a Comment