shija ajipanga kugombea ubunge mwaka 2015 kama mgombea binafsi kutetea wanyama!

Mwigizaji maarufu nchini Deogratious Shija amesema kwamba anajiandaa kugombea ubunge mwaka 2015 kama mgombea binafsi kwa lengo la kutetea wanyama nchini kutokana na mabadiliko ya katiba mpya yanayokuja ambayo kuna vipengele vipya vinavyojadiliwa ili kuruhusu wagombea binafsi ambapo yeye amesema kuwa atatetea wanyama na viumbe wengine ili kupunguza ukatili wa viumbe hai hao hapa nchini.

Akizungumza na bongomovies.com shija amesema ameona ni bora akatetee wanyama maana majimbo yashatetewa sana na viongozi mbalimbali waliopo na waliopita bila mafanikio na huku hali ya majimbo hayo ikuiendelea kuwa duni kila kukicha na anoana ni zamu ya wanyama ambao kwa miaka yote hii hawana mtu wa kuwatetea katika bunge la Tanzania.

"Wanyama ni sehemu ya maisha yetu, ni viumbe kama tulivyo sisi, kuna haja ya kutetea haki zao za msingi aliongeza" shija

"Nimejifunza hili jambo uingereza na kenya nilipotembelea, naamini litafanikiwa nchini" Alimaliza kwa kusema

Post a Comment

 
Top