http://www.kishymba.com/Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja hivi karibuni ameangusha party ya kufuru ya kusherekea siku yake ya kuzaliwa nchini china na party hiyo iliyoanzia hapa Tanzania jijini Dar katika bethidei ya mwanaye (Paula) hivi karibuni ambapo awali alikwenda kutoa misaada ya vitu mbalimbali katika Shule ya Sinza Maalum kisha kuangusha bonge la sherehe katika Hoteli ya Sea Cliff.
Baada ya vurugu hizo ambazo kimsingi zilidaiwa kuteketeza milioni kadhaa, siku chache baadaye (Julai 22, mwaka huu), kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, Kajala alitupia picha za sherehe yake ya kuzaliwa aliyoifanyia nchini China katika Mgahawa wa Waitaly uliyopo Guahnzu.
Chanzo kilichokuwepo katika sherehe hiyo kilisema, Kajala aliwaalika marafiki zake kibao wa nchini humo akiwemo mpenzi wake wa zamani, Petty Man ambapo walikula na kunywa kwa bili yake kitu ambacho wengi walihoji kuhusiana na alikozipata fedha hizo.

“Mh! Si bure kuna kitu, kufanya sherehe katika nchi za watu kama hivi si kitu kidogo lazima uwe na fedha za maana sasa hatujui mwenzetu ameitoa wapi hii jeuri,” alihoji mualikwa mmoja kupitia mitandao ya kijamii.
Kama hiyo haitoshi, shuhuda mwingine aliyechati na mwanahabari wetu alikwenda mbali zaidi kwa kuhoji juu ya kazi zake na pato analoingiza kupitia sinema.

“Nimefuatilia tangu alipoanza kuzitumbua fedha akiwa Bongo hadi huku China, sidhani kama fedha za sinema zinaweza kumpa jeuri hii, kutakuwa na mtu nyuma yake tu,” alisema shuhuda huyo ambaye hakutaka kuchorwa jina gazetini

Post a Comment

 
Top