Siku ya jana Kundi la vijana maarufu kama panya road ambalo ni maarufu kwa kufanya vitendo vya uwizi wa kutimia silaha lilileta hali ya sintofahamu baada ya kuvamia maeneo kadhaa jiji dar na kuiba mali ndani ya maduka na nyumba za watu binafsi, miongoni mwa maeneo yaliathirika ni pamoja na mwananyamala, kinondoni,sinza na ubungo ambapo chanzo cha vurugu hizi kinadaiwa kuwa mwenzao mmoja alipigwa hadi kuuwawa na polisi
Taarifa ya kamanda kova jana usiku ambayo ilirushwa katika kituo cha ITV ambapo katika aliyoyaongea yalikuwa ni haya hapa chini
“Sisi kama Jeshi la Polisi tumepata taarifa vilevile kama walivyopata watu wengine, kwamba hao vijana maarufu kwa jina la ‘Panya Road’ walikuwa wamezagaa maeneo mengi…” Kamanda Kova.
“Hawa ni vijana ambao hawana kazi… hawana maadili mazuri… kwanza tuzungumzie uzito wa tatizo, jinsi ambavyo habari zilivyovuma zimevumishwa kubwa zaidi kuliko uzito wa tukio lenyewe… Nataka niwaambie wananchi kwamba endeleeni na shughuli zenu…”
Hatukatai kwamba hawa vijana wapo.. lakini nasema suala limekuzwa limetiwa hofu, watu wamepata hofu kupindukia …”
Wale wanaopeleka uvumi waache kwa sababu wewe hujaona tukio, ukiletewa message na wewe unampelekea mtu mwingine hiyo sio sahihi…”
Tutashughulikia suala la ‘Panya road’ na leo doria inaendelea usiku kucha, wananchi waondoe hofu wajue jeshi la Polisi lipo… Haiwezekani panya road wakatawala Dar es Salaam… Haiwezekani panya road wawe na nguvu kuliko jeshi la Polisi…”
Wamekamatwa wawili… tuliwakamata muda mfupi tu baada ya kuanza vurugu zao
Unaweza kusikiliza Audio ya taarifa hii hapa chini
Post a Comment