Kuna Msemo unasema Asiyekuwepo na lake halipo , Wengi tunamkumbuka Mwigizaji Marehemu Kanumba alivyobadili mchezo wa Bongo Movies Mpaka kuwa ni Tasnia yenye kukimbiliwa na Wengi ....Sasa Habari tulizozipata ni 
kuwa ile Ofisi yake aliyoiacha baada ya Kufariki Dunia Mama Kanumba na Wadogo zake Walio Ahidi kuiendeleza Wameshindwa na Wameamua Kuifunga baada ya Kukosa Kodi ya kulipia Jengo ...Mama Kanumba amekaririwa akisema kwa sasa Kodi ni laki sita hela ambayo wameshindwa kuilipa kwani Kanumba aliacha Kodi ilikuwa Laki Mbili.

Toka Kanumba Afariki Ofisi hiyo iliweza kutoa Filamu mbili tu na Ambazo Hazikufanya Vizuri sana Katika Soko..

Post a Comment

 
Top