pastor
Matukio ya watumishi wa Mungu kukutwa na skendo za udhalilishaji imekua ikitokea, kama ikitokea huwa inakuwa stori ambayo watu wengi wanazipa attention yani.. Stori ya hivyo inapewa uzito zaidi kutokana na kwamba inakuwa ishu ambayo inahusisha watumishi wa nyumba za ibada.

Nna hii stori kutoka Nigeria, Mchungaji mmoja kaamua kumuandikia mke wake talaka kutokana na kugundua kuwa mke wake ana uhusiano na mchungaji mwenzake ambaye ni rafiki yake wa karibu pia.
Mchungaji Jack aliiambia Mahakama ya Lagos, Nigeria kwamba aligundua uhusiano wa mkewe Kate na mchungaji huyo baada ya kuhama nyumba ambayo walikuwa wakiishi wote tangu mwaka 2011 na hajawahi kurudi tena.
Hata hivyo Kate hakuhudhuria Mahakamani hapo, kuna ripoti zinazosema kwamba mwanamke huyo amefanya kama kususia kuhudhuria kesi hiyo Mahakamahi ambapo Mahakama imetoa amri aandikiwe barua ya kuitwa tena kwenye kesi itakayosikilizwa March 23.

Post a Comment

 
Top