Kutokana na uzushi ulioenea kuwa staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel amejifungua, ndugu, jamaa na marafiki kibao walijazana nyumbani kwake, Mwananyamala jijini Dar es Salaam juzi Alhamisi ili kumpa pongezi, lakini walipokuta habari tofauti walimvaa na kumlaumu kwa kuwadanganya.
Jumatano usiku katika mtandao wa kijamii wa Instagram, msanii Aunt Ezekiel ambaye ni mke wa mtu aliyepata ujauzito mumewe akiwa jela, alitupia picha ikimuonyesha akiwa na kitoto kichanga, ambacho watu wengi waliamini ni wa kwake, hasa kwa vile katika siku za hivi karibuni ameonekana kupunguza mitoko.
Watu wa karibu wa muigizaji huyo ambaye hivi sasa ana uhusiano wa kimapenzi na mcheza shoo wa Diamond Platnumz aitwaye Iyobo, walikwenda nyumbani kwake kwa ajili ya kumpongeza, lakini walipatwa na mshangao baada ya kumkuta akiwa na tumbo lake kama kawaida.
“Sisi tulijua mwenzetu amejaaliwa kujifungua salama, sasa jambo la kushangaza wenzake tumekuja kwa furaha tunakutana na mtu mzima kabisa, hivi aliwaza nini kuweka picha ile katika mtandao na wala asiseme ukweli wa kinachoendelea,” shoga mmoja wa muigizaji huyo aliliambia gazeti hili nje ya nyumba yake, lakini akaomba jina lake lihifadhiwe gazetini.
Mmoja wa marafiki waliodaiwa kufika wakiwa wamekasirika nyumbani kwa Aunt, alikuwa ni shosti yake Wema Sepetu, aliyeshangaa sababu za kutoambiwa mapema kuhusu ukweli wa ishu hiyo.
“Nilishtuka kweli, nikasema inakuwaje Aunt apate mtoto halafu mimi nione kwenye mitandao ya kijamii? Nafika hapa kumbe hamna lolote Aunt naye hakufanya fair bwana,” alisema Aunt.Ujauzito wa Aunt kwa sasa unadaiwa kukaribia mwezi wa saba, hivyo wengi waliposikia amejifungua walidhani amepata kiumbe njiti.
GPL
Post a Comment