Ndani ya saluni hiyo, Polisi walishuhudia mhudumu wa mapokezi ambaye baada ya kuonyeshwa vitambulisho vya askari wa Jeshi la Polisi, alinywea na kuwaruhusu kupekua chumba kimoja baada ya kingine, ili kujionea kama kweli nyumba hiyo ilikuwa ikijihusisha na masuala ya saluni ya uchuaji pekee na siyo vinginevyo.

Katika chumba cha kwanza, askari hao walimkuta mwanaume mmoja akiwa uchi wa nyama, lakini mwanamke aliyekuwa naye akiwa amevaa nguo zake, kitu kilichoashiria kuwa tayari ‘mchezo ulishafanyika’.
  

Katika hali isiyotarajiwa, baada ya kupitia vyumba vingine vinne na kuvikuta tupu, kilichofuata, polisi walishuhudia mwanamke mwenye asili ya Kisomali akiwa uchi na mwanaume wake, dalili zote zikionyesha kuwa walikuwa wakijiandaa kufanya uzinzi.

Baada ya kuwakuta katika hali hiyo, kiongozi wa askari hao, aliwauliza kama hiyo ndiyo biashara ya masaji waliyopata kibali cha kuifanya, lakini wakabakia kujiumauma pasipo kutoa jibu la kueleweka.
 
Binti huyo wa Kisomali, ghafla aliibuka na kuanza kuomba msamaha kwa kitendo hicho, akidai maisha magumu wanayoishi, ndiyo yanayosababisha waifanye biashara hiyo.

Lakini la kushangaza zaidi, ni pale mwanamke huyo alipodai kuwa nyumbani alikotoka, ambako ameolewa, pia alimuacha mwanaye mwenye umri wa miezi minne.
 
Mwanaume aliyekutwa naye, alipoulizwa biashara hiyo inafanyika kwa bei gani, alisema makubaliano yake na mwanamke huyo, ni kutoa kiasi cha shilingi elfu sitini kwa tendo moja!

Post a Comment

 
Top