Mwili wa marehemu ukiwa umewekwa sakafuni kwenye korido kutokana na                 hospitali ya wilaya ya Mbogwe kukosa chumba cha kuhifadhia maiti


Jeshi la polisi wilayani Mbogwe mkoani Geita linashikilia mwalimu wa shule ya msingi Kasandalala wilayani humo Laideth Constantine mwenye umri wa miaka 33 baada ya kumnyonga mwanae wa kiume mwenye umri wa miaka 7 akiwa kwenye nyumba ya kulala wageni (Guest House).

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana ambapo Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita Joseph Konyo amesema tayari wanamshikilia mtuhumiwa baada ya vipimo vya daktari kudhibitisha kuwa mtoto huyo amenyongwa.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema mwalimu huyo amekuwa na mambo ya kushangaza jamii kwani wakati mwingine hujifanya mlokole, mara mkali na kugombana na kila mtu hasa wakati akiwa shuleni.

“Tumekuwa tukimshangaa mwalimu huyu. Kuna wakati anakuwa mlokole, wakati mwingine anakuwa mtaratibu sana, sisi tunashangaa sana kutokea kwa tukio hili,”walisema.

Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mbogwe, Cosmas Kilosa amesema vipimo vinaonesha kuwa mtoto huyo amefariki dunia kwa kunyongwa.

Credit Malunde Blog

Post a Comment

 
Top