Wananchi mkoani Kagera wamepinga uamuzi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumuondoa madarakani Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi na kuwaweka kiporo viongozi wengine walioshiri kuhujumu pesa za akaunti ya Tegeta Escrow.
Nao baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya mkoa huo akiwemo Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kagera, Hamim Mahamoud amepongeza uamuzi wa Rais alioutoa jana kwa kumuondoa kiongozi huyo.
Kwa upande wake, Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Manispaa ya Bukoba, Victor Sherejei akisema kuwa Rais hajatoa uamuzi sahihi. Amemtaka Rais kuwafahamisha Watanzania ni lini pesa za Escrow zitarudishwa katika akaunti hiyo. Akahoji ikiwa kuwaondoa viongozi hao madarakani ndiyo suluhisho la kwamba pesa hizo hazirudishi?
Naye Profesa Anna Tibaijuka amesema baada ya Rais kumuondoa katika nafasi yake aliyokuwa nayo, sasa amerudi jimboni kwake kwa ajili ya kutatua kero na changamoto mbalimbali za wananchi wake kwani nafasi aliyokuwanayo ilikuwa haimpi nafisi ya kuwasimamia wananchi katika jimbo lake na kwamba, pesa hizo alizopewa na Rugemalila zilikuwa za kusaidia shule na alipewa kama zawadi bila kujua kama pesa hizo zilitoka katika akaunti ya Tegeta Escrow, ndiyo maana hakutaka kujiuzulu.
Credit Wavuti
HIVI TUJIULIZE WALIOFURAHIA PROFESA TIBAIJUKA KUVULIWA UWAZIRI WATATEULIWA WAO AU VIPI ILA SIKUPENDA AENGULIWE HADHARANI NI KUTAKA KUMUUA KWA STRESS ILA MUNGU ANALIPA WANAFIKI HAPA HAPA DUNIANI KILA MTU AKIONA HIVI TUJIULIZE WAKATI WA AZIMIO LA ARUSHA NYUMBA ZILIZOTAIFISHWA ZILIKUWA NA THAMANI GANI HIVI DANGOTE ,BILIGET KWAO BILIONI NI HELA NI USHAMBA TU TUKO KWENYE UJENZI WA UBEPARI [ULIMBIKIZAJI WA AWALI] HATUJAFUNULIWA MACHO KUWA NI ENZI ZA UBEPARI UCHWARA NA WATU KAMA MENGI,DEWJI,ROSTAM AZIZ, HIVYO NI VISENTI WAKUBWA WOTE WANAJIFICHA KWENYE MIAVULI YAO WAKIJIDAI TUNAFUNGA MIKANDA SAWA ILA NI UTOTO TUKIKUA TUTAACHA NJIA YA MNAFIKI FUPI TENA SANA WALA TUSITEGEMEE MISAADA KUTOKA G8 KWA KUTIMIZA MAAZIMIO YA BUNGE MABEPARI WANATUSANIFU TU
ReplyDeletewewe uliyeandika hapo jUu ni chizi kama mama yako huyo ungemshauri toka hajachukua hela kuna hela za msaada bila kuomba msaada na kujua chanzo cha hela prof mjinga kama huyo sijui katokea dunia gani wote na wajinga tu
ReplyDelete