Lakini kwa upande wa wanaume mashoga, wao wapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kuupata ugonjwa huu. Sababu kubwa inayotajwa kusababisha hali hii kwa mashoga ni kuwa wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kupata maumivu kwenye tezi dume kutokana na msikusuko unaotokea wakati wa tendo pindi wanapokuwa wanafanya mapenzi haya (athari zipo kwa muingizwaji).
Kati ya mwaka 2005 na 2009 wanaume wapatao 3208 walishiriki utafiti uliofanywa na Taasisi inayojishughulisha na maradhi ya Saratani na kati yao wanaume 1590 waligundulika kuwa na Saratani hii ya Tezi dume.
Utafiti huu ulichapishwa kwenye Jarida la "Cancer Epidemiology".
Marie-Elise Parent, aliyeongoza jopo la watafiti alisema kuwa hii isiwe sababu ya wanaume kuhamasika kuwa na wapenzi wengi.
Pia utafiti huu umeweka wazi kuwa wanaume ambao hawashiriki kabisa tendo la ndoa wako kwenye hatari, mara mbili zaidi ya kawaida kuugua gonjwa hili hatari.
Tafiti zilizotangulia pia zilitanabaisha kuwa kufanya mapenzi mara kwa mara kunapunguza uwezekano wa kuugua Saratani ya Tezi Dume kwa kuwa husaidia kupunguza mrundikano wa wadudu visababishi vya Saratani (carcinogenic crystal-like substances) kwenye tezi dume.
My Take:
Kwa wanaume: Je mwenendo wako unakuweka hatarini au kwenye usalama dhidi ya Tezi dume?
Wamama na wadada, ukiombwa tunda ujue mwenzio anahitaji kinga dhidi ya Saratani. Hivyo msiwe wachoyo.
Na kidume ukiona kila unapoomba tunda unakataliwa basi ujue mwenzio anataka uugue tezi dume.
Kinga ni bora kuliko tiba.
Credit Jamiiforums
Post a Comment