alisema shuhuda huyo akisisitiza si bure paka huyo
alikuwa na kichaa (rabies ) .
Ilifahamika kwamba baada ya paka huyo kumvamia ,
alikimbilia chumba cha matibabu hospitalini hapo
ambapo alipata huduma ya kwanza lakini baada ya
hapo mguu wake ulianza kuvimba . Baada ya
kunyetishiwa ishu hiyo, Ijumaa lilimtafuta Ray C
ambaye alikiri kuvamiwa na kung ’ atwa na paka huyo
huku akipinga madai kwamba labda alitumiwa kichawi .
“Kiukweli naendelea vizuri na jeraha limepona baada ya
kupatiwa matibabu . Watu wanasema sana lakini mimi
sina imani za kichawi , ” alisema Ray C . Maelezo ya
kitaalam yalionesha kwamba endapo Ray C aling ’ atwa
na paka mwenye kichaa , muda wa kupata virusi vya
ugonjwa huo hadi kuanza kwa dalili , kwa kawaida
unaweza kuwa kati ya wiki 3 hadi 12 .
‘ Ray C ’ .
Maelezo hayo ya kitaalam yalieleza kwamba , mara
baada ya kung ’ atwa , Ray C alipaswa kupata chanjo ya
kwanza siku hiyohiyo, chanjo ya pili ilitakiwa iwe
baada ya siku tatu , chanjo ya tatu iwe baada ya siku
saba na chanjo ya mwisho iwe baada ya siku kumi na
nne kama alikuwa hajapata chanjo hiyo kabla .
Kama Ray C aliwahi kuchanjwa dhidi ya ugonjwa huo,
alipaswa apewe chanjo mbili, moja palepale (kinga ) na
nyingine siku ya tatu. Kitaalam ilielezwa kwamba kama
Ray C hatafuata utaratibu huo wa chanjo , atakaa kati ya
siku 21 hadi 90 ambapo dalili za ugonjwa wa kichaa
cha mbwa zitakuwa zimeanza kuonekana , ukijumlisha
na siku saba za kuumwa basi atakiona kifo ndani ya
siku 97 hivyo cha msingi ni kuzingatia chanjo .
Dalili za mtu mwenye ugonjwa huo ambao kiwango cha
kuua ni asilimia 100, ni pamoja na homa kali , kuumwa
kichwa , kuvimba na kuwashwa koo .
Nyingine ni kuwa mwoga , kuchanganyikiwa, kuwa na
tabia zisizo za kawaida , maumivu , kuona vitu ambavyo
havipo (maruweruwe ) , kujifichaficha kwenye kona au
kukimbia , kuogopa maji (hydrophobia ) , mwili kupooza
na kushindwa kula. Nyingine ni mgonjwa kushtushwa
na mwanga na kelele , kupoteza fahamu na mwisho
hupatwa na mauti .
Kwa mujibu wa wataalam hao, muongozo
unaojitosheleza wa kupambana na ugonjwa huo ni
pamoja na kutoa taarifa ya mnyama ( mbwa au paka )
anayehisiwa kuwa na kichaa na kumuangamiza haraka
iwezekanavyo kabla hajasababisha madhara zaidi .
Pia watu wanashauriwa kuwachanja mbwa au paka
wote kwa wakati mmoja na kuendelea kuwachanja
watakaozaliwa huku wakidhibiti mbwa
wanaotangatanga na kuwaua mbwa wote ambao
hawajachanjwa .
Credit: JamiiForums
Post a Comment