Msanii wa R&B kutoka hapa Tanzania Jux ambaye week iliyopita aliachia single yake mpya na video yake inayojulikana kama  ‘Nikuite Nani’ ikiwa imefanyika chini ya mkonowa Director Hanscana sasa bifu limezuka baada ya Director Nisher kumjia juu Hanscana kwa madai kuwa amecopy  idea ya video hiyo kutoka kwenye video ya ‘XO’ ya Joh Makini ambayo alifanya Director Nisher.

Nisher na Hanscana




Nisher leo asubuhi kupitia akaunti yake ya Instagram alipost picha aliyounganisha screenshot za video ya ‘XO’ ya Joh Makini ambayo aliongoza yeye, pamoja na video mpya ya Jux ‘Nikuite Nani’ iliyoongozwa na Hanscana na kuandika 



Joh Makini XO



“Copy, Paste..Why??? Pesa imekuwa Tamu, IDEA na CONCEPT”

 


Katika post nyingine Nisher aliweka screeshot ya video ya Young Dee ‘Kijukuu’, pamoja na video ya Y-Tonny ‘Mama’ iliyofanywa na Hanscana na kuandika “Copy, Paste”.

Hata hivyo post hizo tayari zimefutwa kwenye akaunti ya Nisher.


Haikuishia hapo tu akaunt ya ‘bigbrotherafrica_tanzania_fans’ kwenye Instagram wakapost picha nyingine yenye video ya zamani ya R.Kelly ‘Fiesta’, ambayo shoots zake zinafanana na video zote mbili ya Jux na ya Joh Makini.

Wameandika:

“Have been to this industry for quite sometime kidogo as an observer lakini…. So nkiona vitu Kama hivi always huwa na’smile tu…. smh
@nisherbybee
@hanscana_

Now I don’t know what Y’all gonna say after seeing this!!!!? Video ya Kwanza chini ni video ya R.Kelly ft Jay Z wimbo Fiesta Fiesta ya zamani… With the same background idea
Video ya pili ya katikati ni ya @joh_makini wimbo wa Xo with the same same Background idea
Video ya juu ni ya @juma_jux wimbo wa Nikuite Nani with the very same background idea

Hali ikawa tete mashabiki wakashuka yakwao 

Nani kuchukua idea ya Mwenzie!? Au wote Sawa!? Anyways Big up to @ommydimpoz Kwa Idea nzuri ya video yako.”

Licha ya kwamba Hanscana hajajibu chochote kuhusu kucopy na kupaste, badala yake ameweka orodha ya video tano zinazofata:

“Five Next Videos are u ready for diamondplatnumz are u ready for mauwa sama n ben pol are u ready for nuh mziwanda are u ready for avid n vanessa mdee are u ready for NAVYKENZO are u ready for Bob jr are u ready for Bele 9 …. Uwiiiiiiiiiiiiii ARE U READY”.

Upande wa Nisher baada ya kuachia video ya Fid Q ‘Bongo Hip Hop’, sasa anatarajia kushoot video ya wimbo wa AY ‘Zigo’ itakayofanyika Zanzibar.

Credit Bongo5.com

Post a Comment

 
Top